Header AD

Ukame nchini Kenya sasa ni janga la kitaifa

Mfugaji akiwa mbele ya mifugo yake Kaskazini mwa KenyaN Williams
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa nchi yake inakabiliwa na janga la ukame na kulitangaza sasa ni tatizo la kitaifa.
Hali hii imesababisha maeneo kadhaa ya nchi hiyo yenye uchumi mkubwa Afrika Mashariki kuendelea kukabiliana na janga hili.
Maeneo ambao yameathiriwa ni pamoja na Pwani, Kaskazini na Mashariki mwa nchi hiyo.
Inaelezwa kuwa maeneo hayo yanakabiliwa na uhaba wa chakula, ukosefu wa maji na tayari mamia ya mifugo imepoteza maisha.
Rais Kenyatta amesema serikali yake imeweka mikakati ya kuwasadia watu kutoka maeneo hayo lakini pia ametoa wito kwa wahisani ndani na nje ya nchi hiyo kujitokeza na kusaidia kukabiliana na hali hii.
Tangazo hili linakuja baada ya Umoja wa Mataifa kupitia Shirika lake la chakula FAOkutangaza kuwa Kenya ni mojawapo ya nchi ya barani Afrika inayokabiliwa na tatizo hilo.
Watalaam wanasema, mabadiliko ya hali ya hewa imechangia pakubwa kwa janga hili katika mataifa mengi ya Kusini mwa bara la Afrika.
Ukame nchini Kenya sasa ni janga la kitaifa Ukame nchini Kenya sasa ni janga la kitaifa Reviewed by Unknown on Februari 11, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads