Header AD

FAO: Yemen inakaribia kukumbwa na uhaba mkubwa wa chakula; akiba ya ngano inaelekea kumalizika

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetangaza kuwa, nchi ya Yemen inakaribia kukumbwa na uhaba mkubwa wa chakula kutokana na akiba ya ngano ya nchi hiyo kukaribia kumalizika.

Ripoti kutoka Yemen zinasema kuwa, akiba ya ngano ya nchi hiyo inatarajiwa kumalizika mwezi ujao wa Machi na kwamba, baada ya hapo hali ya chakula ya nchi hiyo itakuwa mbaya mno.
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetangaza katika ripoti yake kwamba, Yemen inakabiliwa na hatari kubwa ya ukosefu wa chakula na kwamba, endapo nchi hiyo haitasaidiwa hali ya chakula nchini Yemen inatarajiwa kuwa mbaya mno katika siku za usoni.
Mwezi uliopita pia, mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya misaada ya kibinadamu nchini Yemen alisisitiza kwamba, akiba ya chakula cha ngano nchini Yemen haitoshelezi isipokuwa kwa kipindi cha miezi mitatu tu.
Uhaba wa chakula unatishia maisha ya maelfu ya raia Yemen
Saudia, kwa kushirikiana na waitifaki wake, ilianzisha hujuma za kila upande dhidi ya Yemen tarehe 26 Machi mwaka 2015 kwa lengo la kumrejesha madarakani kibaraka wake Abdrabbuh Mansur Hadi, rais wa zamani wa Yemen ambaye alijiuzulu nafasi hiyo na kukimbilia Saudia.
Hata hivyo licha ya Riyadh kufanya mauaji na uharibifu mkubwa nchini Yemen, imeshindwa kufikia malengo yake nchini humo. Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama zinakosolewa kwa kutochukua hatua za maana kukomesha mashambulio na jinai za Saudia huko nchini Yemen.
FAO: Yemen inakaribia kukumbwa na uhaba mkubwa wa chakula; akiba ya ngano inaelekea kumalizika FAO: Yemen inakaribia kukumbwa na uhaba mkubwa wa chakula; akiba ya ngano inaelekea kumalizika Reviewed by Unknown on Februari 11, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads