'Fid Q akianzisha label naweza kufanya nae kazi' - Ben Pol.
Kwenye matarajio ya muziki wa Ben Pol kama ukimuuliza hatosita kukwambia kuwa siku moja tutamuona akiwa labda chini ya msanii mwenzake ambaye kwake anaona ataufikisha sehemu nzuri muziki wake wa Rnb.
Kwenye interview yake na XXL ya Clouds FM Ben Pol amesema kuwa >>’Labda Fid Q akiwa na label naweza kufanya naye kazi kwasababu ni mtu ambaye he’s like brother lakini pia ameshafanya vitu vingi bila faida’
‘Naposema bila faida namaanisha ameweza kunishauri ameweza kutoa script kama hivi unapata naye listernling session, anapoteza muda wake na anafanya inamaana huyo mtu ana passion na hicho kitu kesho na keshokutwa ukifanya naye kazi kibiashara rahisi sana’
‘Hela inakuwa siyo kila kitu au hamuwezi kuja kugombana kwasababu ya hela kwasababu ni mtu ambaye ana passion ya hicho kitu na anapenda kuona kitu kiende vizuri hiyo ndo goals bila kutazama kinamlipa au hakimlipi pia ni mtu ambaye ana taste nzuri’. – Ben Pol.
Fid Q asema Cheusi Dawa itakua label tofauti kati ya zote zilizowahi kutokea Bongo
'Fid Q akianzisha label naweza kufanya nae kazi' - Ben Pol.
Reviewed by Unknown
on
Februari 11, 2017
Rating:
Post a Comment