#NIKOHURUBLOG#EDWARD SNOWDEN: “Nilitumia vyanzo huru na vya wazi vya zanatepe (Open Source Software) kama Debian na TOR, sikuwaamini Microsoft”
Edward Snowden alikuwa mtaalamu wa kiufundi wa idara ya Usalama ya Marekani
ijulikanayo kama NSA (National Security Agency) ambaye kwa sasa anaishi nchini
Urusi kwa hifadhi ya kisiasa, alijizolea umaarufu duniani kwa kitendo chake cha
kuvujisha
siri za mifumo ya ufuatiliaji ya kielektroniki ya Marekani na UK (United Kingdom)
maarufu kama “Mass Surveillance” mwaka 2013.
Edward Snowden alisema maneno hayo alipojiunga katika mkutano mkuu wa Free Software Foundation’s LibrePlanet 2016 unaohusisha na kuwaleta pamoja wadau wa mitandao, mafundi wa kielektroniki wa kompyuta na wataalamu wa sheria za mitandaoni kupitia video ya moja kwa moja. Mkutano huo ulifanyika katika Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Massachussetts cha Marekani . Mkutano huu hujadili masuala ya kompyuta na namna ya kutatua matatizo na changamoto wanazozikabili wataalamu wa zanatepe(developers) kuhusiana na masuala ya uwazi na uhuru wa kutumia mitandao bila ya kujulikana(privacy).
Snowden aliongeza kusema kuwa “Ni jambo la wazi kabisa kuwa zanatepe huru naya wazi kabisa (free and transparent software ) inatumiwa na waandishi wengi mno sasa dunia nzima kuhakikisha kuwa serikali mbalimbali haziwezi kuwawinda na kuwadhuru waandishi hawa.” Hii huwezesha uwazi na kumruhusu mwandishi kuangalia sheria mbalimbali za software kabla ya kuitumia ili kuhakikisha ulinzi wa mwandishi na mtaalamu (developer).
Pia Snowden aliongeza kwa kusema “Sikutumia Microsoft katika kufichua siri hizo za ufuatiliaji wa kielektroni unaofanywa na serikali ya Marekani mwaka 2013 kwasababu sikuiamini Microsoft, siyo kwamba nilijua kuwa kuna mlango wa nyuma wanaoutumia microsoft au vitu vifananavyo na hivyo bali tu sikuwa na uhakika sana juu ya Microsoft. Kilichotokea mwaka 2013 kisingetokea bila ya kuwa na Software huru.”
Hii iliibua mashangilio makubwa kutoka kwa waliohudhuria mkutano huo mkubwa.
Mbali na hayo Snowden alitolea mfano juu ya mgongano wa sasa kati ya kampuni ya Apple na Shirika la Upelelezin la Marekani (FBI) huku akisema kuwa huo ni mfano wa kampuni inayojitahidi kusimama kidete kutetea haki za watumiaji wa software yake. Pia Snowden alimalizia kwa kutoa ari kwa wananchi na waajiriwa kote duniani kutotegemea sana kwenye mashirika wanaliyoajiriwa katika kuwatetea bali wao nao wasimame wenyewe.!
Makala kutoka FossBytes
#NIKOHURUBLOG#EDWARD SNOWDEN: “Nilitumia vyanzo huru na vya wazi vya zanatepe (Open Source Software) kama Debian na TOR, sikuwaamini Microsoft”
Reviewed by Unknown
on
Mei 18, 2017
Rating:
Post a Comment