HISTORIA#Historia ya Noti na Sarafu za Tanzania-PART 2
Baada ya kuvunjwa kwa Bodi ya Sarafu ya Afrika ya Mashariki na kuundwa kwa benki kuu za Tanzania, Kenya na Uganda mwaka 1966, Benki Kuu ya Tanzania ilitoa noti za kwanza zenye thamani hizo hizo za Shillingi 5, 10, 20 and Shillingi 100. Upande wa mbele wa noti hizi kulikuwa na
sura ya Mwalimu Nyerere wakati wa kupata uhuru, na upende wa nyuma ulionyesha mambo mbalimbali yaihusuyo Tanzania. Noti ya Shillingi 5 ilikuwa na mlima Kilimanjaro, noti ya shilingi 10 ilikuwa na shamba la mkonge, wakati noti ya shilingi 20 ilikuwa inaonyesha mgodi wa almasi wa Mwadui. Noti ya shillingi mia moja ilikuwa inaonyesha morani wa kimasai akichunga ng'ombe wake.
5 Tz Shilling
10 Tz Shilling
20 Tz Shilling
100 Tz Shilling
Kwa waliotumia noti hizo wanakumbuka kuwa noti ya shilingi kumi ilikuwa inajulikana pia kama jani la katani, wakati ile ya 100 ilikuwa inajulikana pia kama Masai au Pink kutokana na rangi yake. Kwa muda mrefu noti ya shilingi ishirini imeendelea kujulikana kama paund au "mbao" kutokana na historia kuwa mwanzoni ilikuwa ina thamani ya Pound 1.
Hata hivyo sura ya masai kwenye noti ilileta mjadala kidogo kiasi kuwa benki kuu iliamua kuzibadilisha. Ilipofika mwaka 1969, wakatoA noti za shillingi 100 ambazo zilikuwa na wanyama katika mbuga ya serengeti kama ionekanavyo hapa chini
100 Tz Shilling
Noti hizi ziliendelea kutumika hadi mwaka 1978 zilipofanyiwa mabadiliko makubwa hasa ili kuondoa sura ya kitoto ya Nyerere na kuweka picha ya Nyerere akiwa mtu mzima. Noti mpya zote zilikuwa zimendikwa kwa kishwahili tu, na vile vile noti ya shillingi tano ilisimamishwa. Upande wa nyuma wa noti zote kulikuwa na ramani ya Tanzania pamoja na sura mbalimbali zihusuzo Tanzania. Noti ya shillingi 10 ulikuwa na mlima Kilimanjaro, kinyago cha kimakonde na mnara wa Azimio la Arusha; noti ya shillingi ishirini 20 ilikuwa na kiwanda cha nguo kuashiria kuwa nchi ilikuwa inasonga mbele kiviwanda, na ile noti ya shillingi 100 ilikuwa tasisi za elimu kuanzia shule za msingi na vyuo vikuu kuashiria juhudi za nchi kupambana na adui ujinga. Vile vile shughuli za elimu ya kujitegemea zimeonyeshwa kwa wanafunzi kulima kwa jembe la mkono!!
10 Tz Shilling
20 Tz Shilling
100 Tz Shilling
Miaka saba baadaye, mwaka 1985 (muda mfupi sana kabla Nyerere hajastaafu) noti zilifanyiwa mabadiliko tena kwa kuondoa noti ya shillingi 10 na kuwekwa kwa noti ya shillingi 50. Noti hizi zilikuwa na sura ya Nyerere akiwa ameanza kuzeeka, na zilitumia rangi nyingi sana kuliko zilizotangulia. Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1958, noti ya shillingi mia moja ilibadilishwa rangi kutoka "pink" na kuwa ya bluu. Noti ya shilingi ishirini ilionyesha shughuli mbalimbali za baadhi ya viwanda vyetu, wakati shilingi 50 ilionyesha shughuli za kujitolea kujenga mashule. Noti ya shillingi 100 ilionyesha wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaama na baadhi ya majengo ya chuo hico. Nadhani ilikuwa pia kuonyesha kuwa nchi imepiga hatua katika upande wa elimu ya juu.
20 Tz Shilling
50 Tz Shilling
100 Tz Shilling
.... INAENDELEAkwa hisani ya Jamiiforums.com
HISTORIA#Historia ya Noti na Sarafu za Tanzania-PART 2
Reviewed by Unknown
on
Septemba 13, 2016
Rating: 5
Post a Comment