Header AD

HISTORIA#Historia ya Noti na Sarafu za Tanzania-Part 3




Hata hivyo mwaka 1958, noti hizo zilitengezwa upya katika mtindo tofauti na zile zilizokuwapo mwanzo. Noti mpya zilikuwa na rangi nyingi huku zikionyesha mazao mbali mbali ya uchumi yaliyokuwapo Afrika ya Mashariki. Noti ya shillingi 5 ilionyesha pamba na
karafuu; noti ya shillingi 10 ilionyesha mkonge na chai; noti ya shillingi 20 ilionyesha kahawa na alizeti, na mwisho noti ya shillingi 100 ilionyesha minazi, miwese na pareto. Inaelekea kuwa kuanzia hapo, shillingi ya Afrika mashariki iliacha kubebeshwa kwenye pound kwa vile noti mpya hazikuwa na thamani ya pound tena.


5 EA Shilling


10 EA Shilling


20 EA Shilling


100 EA Shilling


Noti hizi ziliendelea hadi baada ya uhuru ingawa mwaka 1961 zilifanyiwa marekebsihao madogo kwenye sura ya mbele ili kuweza kuonyesha sahihi sita za wajumbe wa bodi ya fedha ya afrika mashariki ambapo wakati huo walikuwa wameongezeka na kuwa sita kutoka watano waliokuwapo mwaka 1958. Mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo


5 EA Shilling

10 EA Shilling

20 EA Shilling


100 EA Shilling



Baada ya nchi zote za Afrika ya Mashariki kuwa huru, noti za kwanza zilizotolewa mwaka 1964 zilifanyiwa mabadiliko makubwa sana. Kwanza, noti hizi zilikuwa zimeandikwa katika kiingereza, kiarabu na kishwahili; halafu sura ya mtawala wa uingereza iliondolewa na badala yake kuwekwa mashua. Sikuweza kufahamu mara moja kwa nini waliamua kutumia mashua. Sura za nyuma za noti ziliendelea kuonyesha mazao mbalimbali ya Afrika ya Mashariki ingawa kwa mpangilio tofauti kama inonekanavyo katika picha hizi.


5 EA Shilling

10 EA Shilling

20 EA Shilling

100 EA Shilling




..... INAENDELEA
HISTORIA#Historia ya Noti na Sarafu za Tanzania-Part 3 HISTORIA#Historia ya Noti na Sarafu za Tanzania-Part 3 Reviewed by Unknown on Septemba 13, 2016 Rating: 5

Post AD

Propellerads