Header AD

HISTORIA#Historia ya Noti na Sarafu za Tanzania--PART 4



Mwishoni mwa mwaka 1985 Nyerere alirudi kijijini kwake Butiama na kuiacha Ikulu mikononi mwa Mwinyi. Noti mpya zilizotolewa mwishoni mwa mwaka 1986 zilikuwa sawa kabisa na zile zilizoacha na Nyerere isipokuwa zilikuwa na sura ya Mwinyi isipokuwa noti zile za Shillingi 100 ambazo ziliendelea kuwa na sura ya Nyerere kama Baba wa Taifa. Vile vile noti mpya ya shillingi 200 ilianzishwa ikiwa inajulika wakati huo kama "double cabin." Nyuma ya noti hizi za Shillingi 200 kulikuwa na wavuvi wanaodhaniwa kuwa walikuwa wa Zanzibar kwa vile kuna karafuu inayoonekana kwa pembeni.

20 Tz Shilling

50 Tz Shilling

100 Tz Shilling

200 Tz Shilling


Ilipofika mwaka 1988, kufuatia kushuka kwa thamani ya shilingi, ilikuwa ni muhimu kuwepo kwa noti zenye thamani kubwa zaidi ili kuwapunguzia watu mzigo wa pesa. Hivyo benki kuu ikaanzisha noti mpya za shillingi 500, ambao zilijulikana kama "Pajero." Noti hizi za shillingi 500 zilikuwa na sura tofauti kabisa na zile nyingine. Nembo ya Taifa ilikuwa ya rangi, halafu zilikuwa na nembo ya waziwazi ya Benki Kuu ya Tanzania. Nyuma yake zilionyesha akina mama wakivuna zao la kahawa au karafuu, sikumbuki tafsri ya picha hiyo vizuri.


500 Tz Shilling


Kasi ya kupungua kwa thamani ya shilingi ilikuwa kali sana kiasi kuwa miaka miwili baadaye, Benki Kuu ililazimika kuingiza noti mpya ya Shillingi 1000 ambayo ilikuwa na sura kama ile ya Shillingi 500 isipokuwa ngao ya taifa haikuwa ya rangi. Vile vile ilikuwa na maandishi ya ndani kwa ndani kuonyesha 1000. Nyuma yake kulikuwa kiwanda cha nyama cha Tanganyika packers cha pale Kawe.


1000 Tz Shilling




Noti zetu wakati huo zilikuwa pana sana na zilikuwa zinaongezeka upana kadiri thamani yake inavyopanda. Ilipofika mwaka 1992, Benki kuu ilifanya mabadiliko makubwa katika noti zetu. Kwanza zilipunguzwa sana upana halafu zote zikatengezwa upya kuwa na sura inayofanana. Noti ya shillingi 20 iliachisHwa na badala yake zikaongezwa noti mbili za Shillingi 5,000 na Shillingi 10,000 kama ifuatavyo:


50 Tz Shilling



100 Tz Shilling

 

200 Tz Shilling

500 Tz Shilling

 

1000 Tz Shilling

5000 Tz Shilling

10000 Tz Shilling


Noti hizi ziliendelea kutumiwa hadi mwisho wa utawala wa Mwinyi mwaka 1995.

......INAENDELEA

source:jamiiforums 
HISTORIA#Historia ya Noti na Sarafu za Tanzania--PART 4 HISTORIA#Historia ya Noti na Sarafu za Tanzania--PART 4 Reviewed by Unknown on Septemba 13, 2016 Rating: 5

Post AD

Propellerads