Header AD

NIKOHURU BLOG#Air Tanzania kuja na ushindani mkubwa – Wizara ya Uchukuzi*

freevector-air-tanzania
Serikali imedai kuwa shirika la ndege la Tanzania (Air Tanzania) linakuja na ushindano mkubwa kwenye biashara ya usafiri wa ndege.Kauli hiyo imetolewa leo na
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi. Edwin A. Ngonyani wakati akijibu swali bungeni lililohusiana na gharama za usafiri wa anga nchini.
Alisema serikali iliruhusu kuwepo kwa ushindani wa biashara ya usafiri wa anga na kuyapa makampuni uhuru wa kupanga bei zake.
“Tuliamua tena kupitia bunge hili hili kwamba turuhusu ushindani na ndivyo tulivyofanya, kupanga viwango kwa mamlaka zetu maana yake ni kutoka katika mipango tuliyoipanga hapo awali,” alisema.

Aliongeza kuwa ujio mpya wa Air Tanzania unaweza ukasababisha kushuka kwa gharama za usafiri huo kutokana na changamoto itakazozileta.
“Mimi sina matatizo kama bunge hili na serikali kwa ujumla itaamua, lakini kwa maoni yangu ni vema, ngoja tuimarishe shirika letu la ndege la Air Tanzania kama mnavyofahamu limeanza kulimarika litaingiza ushindani mkubwa na mimi nina uhakika hao sasa hivi walioweka viwango vya juu watalazimika kuvishusha ama kuondoka katika biashara hiyo na kuliacha shirika likitamba.
BY: EMMY MWAIPOPO
NIKOHURU BLOG#Air Tanzania kuja na ushindani mkubwa – Wizara ya Uchukuzi* NIKOHURU BLOG#Air Tanzania kuja na ushindani mkubwa – Wizara ya Uchukuzi* Reviewed by Unknown on Septemba 15, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads