Header AD

NIKOHURU BLOG#Wema Sepetu Ajipanga kumfikisha Diamond Mahakamani

Msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu anaandaa utaratibu wa kumfikisha mahakamani aliyekuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kufuatia kitendo cha msanii wa Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Raymond ‘Rayvanny’ kumtumia kwenye video ya wimbo wake wa Natafuta Kiki bila makubaliano. 
Akizungumza nasi hivi karibuni, Wema alisema amefikia uamuzi huo kutokana na Diamond kukiuka makubaliano waliyofanya awali kuhusu yeye kuonekana kwenye video hiyo. Alisema: “Diamond alinifuata na kunitaka nionekane kwenye video ya msanii wake Raymond, nikamwambia anipe milioni 10, yeye akaonesha alikuwa anataka free huku akisema mbona nilimsaidia Ommy Dimpoz.
“Nilimwambia kuwa nilimsaidia Dimpoz kwa kuwa alikuwa anahitaji msaada lakini yeye nilitaka anipe kiasi hicho cha pesa. “Baadaye niliongea na Martin Kadinda kuhusu kile alichotaka Diamond na pesa ambayo nilimtajia, Martin akaniambia kwa ishu hiyo hata milioni 10 ni ndogo, nikashituka na ndiyo maana hata Diamond aliponipigia tena kuhusu ishu hiyo nilimchomolea.” Wema akaendelea kudai kuwa, licha ya kwamba yeye alishakataa kuonekana kwenye video hiyo, siku ya ‘bethidei’ ya Rommy Jones alifanyiwa kitendo ambacho si cha haki
“Nikiwa pale kwenye ‘bethidei’ ya Rommy, bila kujua wana lao jambo, Raymond akawa anajiweka sana kwangu huku video na picha mbalimbali zikichukuliwa, sikujua kwamba kuna kitu nyuma yake, ile video ilipotoka nikashangaa nimetumika bila ridhaa yangu.

 “Ndiyo maana nimewasiliana na wanasheria wangu ili nimshitaki Diamond kwani yeye ndiye niliyezungumza naye na tukashindwana,” alisema Wema. Kufuatia tuhuma hizo, Risasi lilifanya jitihada za kuwatafuta Diamond na Raymond  ili kuzungumzia madai hayo lakini hawakuweza kupatikana mara moja. 

Alipotafutwa meneja wa Diamond, Salam Sharraf alisema: “Mimi sidhani kama kuna ishu hapo maana hata baada ya ile ‘bethidei’ ya Rommy, Wema aliiposti ile video kwenye ukurasa wake wa Insta kuonesha kuwa hakuwa na shida na sisi tukajua hata kwenye kuonekana kwenye ile video si tatizo.”

Angalia NATAFUTA KIKI YA RAY VANNY



Source#ubuyublog
NIKOHURU BLOG#Wema Sepetu Ajipanga kumfikisha Diamond Mahakamani NIKOHURU BLOG#Wema Sepetu Ajipanga kumfikisha Diamond Mahakamani Reviewed by Unknown on Septemba 17, 2016 Rating: 5

Maoni 1

  1. Mimi ni Black Rambo kutoka Grammy, ninafanya kazi katika Kambi ya Grammy, mke wangu alifariki mwaka 6 iliyopita na tangu nimekuwa nikimtunza mwanangu pekee aitwaye Clinton, rafiki yangu wa ushauri wangu wa kumtafuta mke, kwenye upekuzi wangu nilikutana na Jennifer alikuwa na mwanamke wa Kiingereza, Nilimpenda sana kiasi kwamba ningeweza kumpa kila kitu alichokuwa na umri wa miaka 37, baada ya muda fulani wa uchumba nilikuwa na mapenzi sana naye, tulikuwa na kutokuelewana, na alivunja na mimi na ninamsihi arudi mwanangu aitwaye alisema Hapana, kwamba amempata mtu mwingine, na tunapendana sana baada ya siku kadhaa nilisoma makala kuhusu jinsi Dk Lomin anaweza kusaidiana , Niliamua kutoa jaribu, nawasiliana na Dk Lomi kwa msaada aliniambia nini cha kufanya ili kumrudisha mpenzi wangu niliyefanya, alifanya maombi na Jennifer alikuwa nyuma ananipenda na kunithamini zaidi sasa, na tuna wakati mzuri wa maisha yetu, Dk Lomi pia kuandaa baadhi ya mimea ya asili ambayo imenifanya niwe na nguvu na afya tena sasa nahisi kama kijana niliyemridhisha vizuri sana sisi sote tuna furaha, wasiliana na Dk Lomi kwenye WhatsApp namba +2349034287285 au barua pepe yake kwenye lomiultimatetemple@gmail.com ANA SULUHISHO BORA KWAKO.

    JibuFuta

Post AD

Propellerads