Donald Trump afuata nyayo za Magufuli
Rais mteule Marekani ameonekana kufuata nyayo za Magufuli katika kuwatumikia wananchi.Rais John Pombe Magufuli ni rais anayekosa usingizi kwa kupigania maisha ya wanyonge bila kutaka kuwafurahisha baadhi ya watu.Tabia hii hata Trump anayo.
Kuna maeneo mengi misimamo ya viongozi hawa inafanana.Hii ni mifano michache..
1.KUBANA MATUMIZI
Viongozi wote hawa wameonesha nia ya kubana matumizi.JPM; ameokoa pesa nyingi holela kama safari za nje, posho, sherehe zisizo na tija na matumizi mengine holela, pesa hizi zimeelekezwa kwenye maendeleo .Trump; amezuia pendekezo la kununua ndege mpya ya rais yenye thamani ya trillion 8 za Kitanzania , pia anafikiria USA kuacha kutoa pesa kwa majeshi ya NATO.
2.UCHOCHEZI WA VYOMBO VYA HABARI
Viongozi wote hawa wanakerwa na uzushi na uchochezi wa vyombo vya habari katika nchi zao.Tumeona JPM alivyokerwa na magazeti mawili yanayohatarisha mustakabali ya amani yetu akiwa ziarani Shinyanga.Hali hiyo pia tumeiona kwa Trump alipokuwa anaongea na waandishi wa habari kwa kukituhumu kituo cha televisheni cha CNN kwa kutoa HABARI za uongo na uzushi.
3.KUSIMAMIA UKWELI NA KUJIAMINI.
Viongozi wote hawa hawana unafiki wala hawafanyi kazi ili wapendwe.Mara nyingi husimamia haki na ukweli.JPM ; amejitoa kupigania maisha ya Watanzania masikini, amekuwa mkweli siku zote na wala haongozi nchi kuwaridhisha mafisadi wachache na kuwaumiza wananchi wengi.Siku zote yeye husema ukweli.Trump; yeye pia hataki ujinga amekuwa akitoa kauli zenye ukweli kwa mustakabali wa Wamarekani.
4.VIWANDA NA UWEKEZAJI
Viongozi wote hawa wana nia thabiti ya nchi zao ziwe na viwanda vingi.JPM; ameweka mazingira rafiki kwa wawekezaji kujenga viwanda vingi , vile vile kuwa na mipango ya kuzuia kuingia bidhaa kuingia nchini kiholela .Trump; amepinga hatua ya wawekezaji kujenga viwanda Mexico ili wapate cheap labour na kuifanya Marekani soko la bidhaa zinazotengenezwa Mexico.
Kwa hiyo inabidi viongozi hawa wawe karibu sana kwani wote wana sifa zinazofanana katika kuwatumikia wananchi wanyonge.
Donald Trump afuata nyayo za Magufuli
Reviewed by Unknown
on
Januari 15, 2017
Rating:
Post a Comment