Header AD

Utafiti: Mabilionea 8 wanaoimiliki Dunia

Orodha ya mabilionea ya Forbes, Machi 2016

Takwimu za shirika hilo, ambazo zimepingwa na baadhi ya wakosoaji, zinatokana na maelezo na habari za kina zilizokusanywa na shirika hilo, na zinaonesha pengo kati ya matajiri na maskini ni kubwa “kuliko ilivyodhaniwa awali”.

Ripoti hiyo ya Oxfam imetolewa wakati mkutano mkubwa kuhusu uchumi wa dunia unaanza mjini Davos.
Mark Littlewood, wa Taasisi ya Masuala ya Uchumi, amesema Oxfam badala yake wanafaa kuangazia njia ya kusisimua ukuaji.

“Kama shirika linalopiga vita umaskini, Oxfam wanaonekana sana kuangazia zaidi matajiri,” mkurugenzi mkuu huyo wa shirika hilo la ushauri amesema.

Kwa wale ambao wana malengo ya “kuangamiza kabisa umaskini uliokithiri”, sana wanafaa kuangazia hatua za kusisimua ukuaji wa uchumi, ameongeza.

Ben Southwood, ambaye ni mkuu wa utafiri katika Taasisi ya Adam Smith, amesema la muhimu zaidi si kiasi cha mali inayomilikiwa na watu matajiri zaidi duniani, bali ni hali ya maisha ya watu maskini zaidi duniani, ambayo inaimarika mwaka baada ya mwaka.

“Kila mwaka, tunapotoshwa na takwimu za Oxfam. Takwimu ziko sawa – zinatoka kwa Credit Suisse – lakini ufasiri wa takwimu hizo si sahihi.”

Baadhi ya watu wanane matajiri zaidi duniani hata hivyo wamekuwa wakitoa mabilioni ya dola kama hisani.

Mwaka 2000 Bill Gates na mkewe Melinda walianzisha wakfu ambao wameupatia zaidi ya $44bn.

Mwaka 2015 Mark Zuckerberg na mkewe Priscilla Chan waliahidi kutoa 99% ya utajiri wao, ambao ulikuwa sawa na $45bn kwa makadirio ya thamani ya hisa za Facebook wakati huo.

Source:BBC
Utafiti: Mabilionea 8 wanaoimiliki Dunia Utafiti: Mabilionea 8 wanaoimiliki Dunia Reviewed by Unknown on Januari 16, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads