Header AD

Wanafunzi 58 wafutiwa matokeo kwa udanganyifu

BARAZA la Mitihani (Necta), limefuta matokeo ya watahiniwa 58 wa kidato cha pili na darasa la nne, waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani ya upimaji wa kitaifa iliyofanyika Novemba mwaka jana.



Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde, alisema licha ya udanganyifu huo watahiniwa hao wataruhusiwa kurudia mitihani hiyo.

Katika mtihani wa taifa wa kumaliza darasa la saba wa Oktoba mwaka jana, watahiniwa 238 walifutiwa matokeo kutokana na kuhusika na udanganyifu.

Necta ilizitaja shule zilizohusika na udanganyifu huo na wilaya zake kwenye mabano kuwa ni Tumaini (Sengerema), Little Flower (Serengeti), St. Getrude (Madaba Ruvuma), Mihamakumi, Kondi, Kasandalala (Sikonge-Tabora) na Qash (Babati).

Source: Nipashe

Wanafunzi 58 wafutiwa matokeo kwa udanganyifu Wanafunzi 58 wafutiwa matokeo kwa udanganyifu Reviewed by Unknown on Januari 16, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads