NIKOHURU BLOG# Wakimbizi wa Sudan Kusini wafika milioni moja
Umoja wa Mataifa unasema kuwa idadi ya watu waliokimbia nchi ya Sudan Kusini kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo imepita watu milioni moja
.
.
Idadi hiyo inajumuisha zaidi ya watu 185,000 ambao wameikimbia nchi kufuatia mapigano mapya yaliyoanza mwezi Julai.
Zaidi ya watu milioni 1.6 nao wamelazimika kuhama makwao ndani ya Sudan Kusini.
Kati ya hao wakimbizi 373,626 wameingia nchini Uganga huku theluthi moja kati yao wakiwasili tangu mwezi Julai na 20,000 wiki iliyopita. Wale wanaowasili sasa wanasema kuwa kuna mapigano mapya huku raia wakishambuliwa na makundi yaliyojihami ambayo hupora, huwadhulumu kimapenzi wanawake na wasichana na kuwaingiza jeshini vijana wa kiume.
Wakimbizi 292,000 waliingia nchini Ethiopia huku 11,000 wakivuka na kungia Gambella wiki iliyopita. Wale wanaowsili kwa sasa wanatoka jamii ya Nuer wakiwemo watoto 500 wasioandana na wazazi.
247,317 wamewasili nchini Sudan, 1800 wakiwasili kila mwezi katika jimbo la White Nile na mafuriko yakiwazuia wengine.
Nchini Kenya wakimbizi 90,000 wamewasili nao wengine 300 wanawasili kila wiki kutokana na sababu za kiusalama, uchumi mbaya na ukame.
Wakimbizi 40,000 wamesili nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo katika mkoa wa Ituri.
Wakimbizi wengi wanoawasili nchini Uganda ambayo inawapa makao wakimbizi wengi kutoka Sudan Kusini, wanaonekana wamechoka baada ya kutembea siku kadha msituni bila chakula wala maji.
Tofauti kati ya Rais Salva Kiir na aliyekuwa makamu wa Rais Riek Machar zilisababisha kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwezi Disemba mwaka 2013.
Makadirio ya idadi ya watu nchini Sudan Kusini ni kati ya watu milioni 10 hadi milioni 12. Hii inamaaanisha kuwa takriban asilimia 20 ya watu hao hawana makao kutokana na mzozo uliopo.
BBC,com
BBC,com
NIKOHURU BLOG# Wakimbizi wa Sudan Kusini wafika milioni moja
Reviewed by Unknown
on
Septemba 17, 2016
Rating:
Post a Comment