Header AD

TAMKO LA MAALIM SEIF UN KUJA NA VIKWAZO HIVI KWA TANZANIA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amepokea tamko la maandishi kutoka Muungano wa Vyama vya Kiliberali Duniani kupitia Kikao cha 33 cha Baraza la Haki za Binaadamu juu ya mkwamo wa kisiasa visiwani Zanzibar.Tamko hilo ambalo lilipelekwa na aliekuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia CUF Maalim Seif 

Sharif Hamad akiwa ziarani Marekani, nchi za ulaya, Canada na Umoja wa mataifa lilichapishwa katika tovuti ya LI limelitaka baraza la umoja wa mataifa kuchukua hatua kali ili kukomesha uvunjwaji mkubwa wa haki za binadamu na ukandamizwaji wa haki za kisiasa na raia visiwani Zanzibar.

Kwa hali jinsi ilivyo Tanzania iko hatarini kuwekewa vikwazo vya kisiasa na zuio la kusafiri kwa baadhi ya viongozi wake baada ya taasisi ya kimataifa ya umoja wa wanaliberali(Liberal International) kuliandikia barua baraza la haki za binadamu la umoja wa mataifa (UNHRC) ambapo katika barua hiyo LI ilitaka jumuiya za kimataifa kufikiria kuiwekea vikwazo nchi ya Tanzania ikiwa ni kuzuia kusafiri na kuzuia mali zote za walioshiriki kuidhinisha vitendo vya utesaji wa wanasiasa wa upinzani.

TAMKO LA MAALIM SEIF UN KUJA NA VIKWAZO HIVI KWA TANZANIA TAMKO LA MAALIM SEIF UN KUJA NA VIKWAZO HIVI KWA TANZANIA Reviewed by Unknown on Septemba 21, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads