Header AD

Terry kuwavaa Arsenal wikiendi hii


Beki wa Chelsea John Terry amerejea mazoezini baada ya kupata majeraha yalimweka nje kwa takriban wiki moja na nusu na anatarajiwa kuiongoza timu hiyo kwenye mchezo dhidi ya mahimu wao Arsenal utakaopigwa
Jumamosi wikiende hii.
Nahodha huyo wa Chelsea aliukosa mchezo wa nyumbani waliofungwa magoli 2-1 dhidi ya Liverpool Ijumaa baada ya kupata jeraha la kifundo cha mguu kwenye mchezo ulioisha kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Swansea
.
Nohodha huyo wa zamani wa England hatacheza mchezo wa Kombe la EFL dhidi ya Leicester utakaochezwa leo usiku.
Meneja Antonio Conte amesema: ‘Tumesikitishwa sana na kipigo dhidi ya Liverpool lakini nashukuru tumerekebisha makosa yetu na nimeona ari waliyonayo vijana mazoezini. Ni suala zuri sana.
‘Ni wiki ngumu hii kwasababu tunaenda kupambana na timu mbili kubwa. Leicester walishinda ubingwa msimu uliopita na Arsenal ni timu kubwa ambayo inawania ubingwa msimu huu. Ni wiki ngumu hii lakini tuko tayari.’
Terry kuwavaa Arsenal wikiendi hii Terry kuwavaa Arsenal wikiendi hii Reviewed by Unknown on Septemba 20, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads