Header AD

UCHUMI#Msemakweli ni mpenzi wa Mungu: Uchumi bado haujaporomoka

Tuache mihemko kwa kauli za wanasiasa eti uchumi umeporomoka huu ni uongo. Maisha ni ya kawaida kabisa hakuna kilichobadilika kwa mtanzania wa kawaida.

1. Shilingi haijaporomoka dhidi ya dola
2. Bei za vyakula sokono ni zile zile
3. Kodi za nyumba ni zile zile
3. Watu wanaokula mlo mmoja kwa siku wastani ni ule ule
4. Mishahara kwa watumishi almost ni ile ile
5. Kusema ukweli bei ya basic needs ni ile ile mabadiliko ni madogo sana vingine vimepanda vingine vimeshuka
6. Upatikanaji wa pembejeo kwa mkulima ni ule ule
7.........

Tatizo lililopo ni wachache waliokuwa wanaishi kijanja janja wameishiwa hawana ujanja wa kutoa offer zisizo na kichwa wala miguu wanataka kugeneralize uchumi umeporomoka. Hawana tena uwezo wa kumnunua kuku sh 500,000 kwenye minada makanisani au kuandaa futari kipindi cha mfungo. Hawawezi mwezi mzima kutoa offer bar, kuandaa birthdays, kitchen party, n.k.

Wapinzani wameshindwa kuaddress matatizo ya msingi yanayomtesa mtanzania kama elimu bora, mfumo wa afya, uhakika wa milo mitatu kwa siku, miundombinu, n.k. hawana tena hoja ya msingi vita dhidi ya ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali za umma. Wao wamejikita na jambo la kipuuzi eti UKUTA

CCM nao kupambana na ufisadi kwao ni tamthilia ya kusadikika.. Wanachokifanya ni kucheza na akili za wanao watawala.. Wamejificha kwenye kichaka cha mamvi na kuwaaminisha wasiojielewa ufisadi kwao umekwisha wakati limebaki lundo la mafisadi linawamiliki

Hapa cha muhimu ni kuitathmini dhamira ya dhati ya JPM tumsaidie coz wapinzani hawana dhamira ya dhati zaidi ya madaraka hata CCM kama chama nao hawana dhamira ya dhati wanaombea hata leo jamaa azimike waweke mtu atayelinda maslahi yao

Ni kweli kuna maeneo JPM anachemka lakini ni madogo ukilinganisha na maeneo aliyofanya vizuri. Anapokosea tusisite kumrekebisha hata kama tunahisi ana kiburi. Watanzania wa kawaida tumuunge mkono kwani akishindwa hajashindwa JPM tumeshindwa watanzania na tunao pata tabu ni sisi

Kwa hisani ya: www.jamiiforums.com
UCHUMI#Msemakweli ni mpenzi wa Mungu: Uchumi bado haujaporomoka UCHUMI#Msemakweli ni mpenzi wa Mungu: Uchumi bado haujaporomoka Reviewed by Unknown on Septemba 12, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads