Jina la wizara latumika kutapeli wafanyabiashara
Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) wilayani hapa, umesema kumeibuka matapeli wanaotumia jina la Wizara ya Maliasili na Utalii kuwatapeli wafanyabiashara wa mazao ya misitu.
Meneja wa TFS Wilaya ya Kibaha, Peter Nyahende ametaja eneo lililoshamiri kwa utapeli wa aina hiyo kuwa ni Barabara Kuu ya Morogoro- Dar es Salaam, hususan Maili Moja na kwamba watu hao wamekuwa wakijiita Paruanji.
Nyahende alisema watu hao pia hujifanya ni maofisa misitu na kuwatapeli wafanyabiashara wasiofuata utaratibu wa usafirishaji na kuchukua fedha badala ya kuwafikisha kwenye vyombo vya dola.
Alisema wafanyabiashara hao bila kujua wametapeliwa, hukumbana na mkono wa sheria baadaye wanapokutana na maofisa Maliasili halisi.
Jina la wizara latumika kutapeli wafanyabiashara
Reviewed by Unknown
on
Oktoba 21, 2016
Rating:
Post a Comment