Vikosi vya Iraq vyakaribia kuudhibiti mji wa Mosul
Vikosi vya Iraq sasa vimebaki kilomita moja tu kudhibiti mji wa Mosul, mji wa mwisho kwa ukubwa nchini humo bado unadhibitiwa na wapiganaji wa Islamic State.
Vikosi maalum vinaelekea katika mji wa Mosul kutoka Mashariki walifanya mashambulizi kabla ya alfajiri.
Mwandishi wa BBC anayesafiri na safu ya kivita alisema wamekuwa wakilengwa mara kwa mara na wapiganaji wa kundi la IS waliokuwa wakiendesha magari yaliotegeshwa mabomu.
Lakini bado mafanikio ni makubwa na vikosi vya serikali vimesonga mbele hadi kijiji cha Bazwaya, nje kidogo ya mji wa Mosul.
Vikosi vya Iraq vyakaribia kuudhibiti mji wa Mosul
Reviewed by Unknown
on
Novemba 01, 2016
Rating:
Post a Comment