NIKOHURU BLOG#Dawa ya mpango wa uzazi kwa wanaume
Dawa inayotolewa kwa njiya ya sindano imetajwa kama mafanikio makubwa ya njiya ya mpango wa uzazi miongoni mwa wanaume.Watafiti kutoka Marekani wamesema dawa hiyo imefikia asili mia 96 ya mafanikio baada ya kufanyiwa majaribio miongoni mwa wanaume 270.
Kati ya wanaume hao ni wanne pekee walioweza kuwafanya wenzi zao kutunga mimba. Hata hivyo dawa hiyo imeripotiwa kuwa madhara mengi miongoni mwa wanaume ikiwemo vipele usoni na kuwa na usununu. Watafiti wamekua wakitafuta dawa ya kupanga uzazi ya wanaume kwa miaka 20.
Wataalamu hao wamekua wakitafuta jinsi ya kupunguza idadi ya manii bila kusababisha madhara ya uzazi. Kimaumbile wanaume hutoa manii kila wakati na wanasayansi wamekua wakitaka kupunguza idadi kutoka milioni 15 hadi milioni moja.
Utafiti wa dawa hii ulilenga wanaume kati ya umri wa miaka 18 hadi 45, na walio na uhusiano na mwenzi mmoja wa kike. Walishiriki kwenye utafiti huo kwa mwaka mmoja. Walidungwa sindano hiyo na kupunguza idadi ya manii hadi milioni moja. Kisha hawakupokea dawa hiyo ili kubaini kasi ya kuongezeka kwa manii yao hadi milioni 15.
Baadhi walisema iliwachukua mwaka mmoja kabla ya idadi kamili na inayotakikana kurudi. Baadhi ya madhara kama vile mfadhaiko, usununu, vipele usoni na maumivu ya misuli yalisababisha wanaume 20 kujitoa kwenye utafiti. Mtafiti mkuu wa dawa hii Dkt. Festin amesema wanaangazia njiya nyingine ya kuboresha dawa hiyo ikiwemo kuiotoa kama mafuta.
NIKOHURU BLOG#Dawa ya mpango wa uzazi kwa wanaume
Reviewed by Unknown
on
Novemba 01, 2016
Rating:
Post a Comment