Header AD

Wataalam wa afya kuanza kusajiliwa na kupewa leseni

Wataalamu mbalimbali wa sekta ya afya, sasa wataanza kusajiliwa na kupewa leseni zitakazowatambulisha na zitakuwa na masharti maalumu.

Hayo yamesema na Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Muhammad Kambi  jana Jumatano  jijini Dar es salaam, wakati akifungua mkutano wa mwaka wa Chama cha Wafiziotherapia (APTA).

Alisema serikali imeanza mchakato wa kuipitia upya Sheria ya Madaktari wa Tanganyika, ambayo itaongezwa sharti hilo pamoja na kuundwa kwa bodi maalumu itakayosimamia maadili ya watumishi hao.

“Lakini hivi sasa kuna taaluma nyingi ndani ya hii fani, kwa mfano ninyi wataalamu wa fiziotherapia. Mpo lakini sheria haiwatambui, kwa maana hiyo inakuwa vigumu hata kuwafuatilia. Ndiyo msingi wa kuipitia upya sheria hii,” alisema.

“Katika sheria mpya itakayoboreshwa, kila mtumishi atatakiwa kukata leseni. Kila mtumishi atatakiwa kujiendeleza kielimu, kuongeza ujuzi ili aendane na wakati uliopo kwa sababu mambo yanabadilika, kile ulichosoma jana unahitaji kujifunza zaidi,” alisema.

Aidha Kambi alisema tayari maboresho ya sheria hiyo yameshawasilishwa katika Kamati ya Baraza la Mawaziri ya Katiba na Sheria na imeshapitiwa.
Wataalam wa afya kuanza kusajiliwa na kupewa leseni Wataalam wa afya kuanza kusajiliwa na kupewa leseni Reviewed by Unknown on Novemba 24, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads