CRISTIANO RONALDO sasa kuwania tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka wa LAUREUS WORLD SPORTS
Mambo yanazidi kuwa mazuri kwa mwanasoka wa Real madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo ambaye ametajwa kuwania tuzo ya mwanamichezo bora wa Laureus shirika linalojihusisha na
Academy za michezo duniani na ugawaji tuzo katika kada mbalimbali za michezo.
Wapigaji kura katika tuzo hizo ambao ni waandishi wa habari za michezo kimataifa watashiriki kupiga kura. Wanaowania tuzo hizi ni kijana wa kireno Cristian Ronaldo, wagombea wenza ambao ni mchezaji wa mpira wa kikapu Steph Curry na LeBron James, wanariadha Usain Bolt na Mo Farah na mcheza Tenisi Andy Murray.
Ronaldo atakuwa mwanasoka wa kwanza kuwania tunzo hii toka zilipoanzishwa mnamo mwaka 2000, japokuwa hapo nyuma aliwahi kuwania tuzo hizi mara 3 katika nyanja zingine na kuambulia patupu.
CRISTIANO RONALDO sasa kuwania tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka wa LAUREUS WORLD SPORTS
Reviewed by Unknown
on
Januari 11, 2017
Rating:
Post a Comment