Header AD

Sanamu la MESSI lavunjwa huko ARGENTINA


Sanamu ya mwanasoka nyota wa BARCELONA na Nahodha wa timu ya taifa ya ARGENTINA Lionel Messi lavunjwa nusu kwa nusu huko Buenos Aires.

Sanamu hiyo ilitengenezwa mahsusi kabisa kwa ajili ya kumshawishi MESSI kurudi tena kuitumikia timu yake ya taifa ARGRNTINA. Hii ni baada ya MESSI kutangaza kustaafu kucheza timu ya taifa baada tu ya fainali za COPA AMERICA kumalizika mwaka jana.

Sanamu hiyo iliyohujumiwa kwa kuvunjwa tayari mipango kwa ajili ya kuitengeneza upya ishaanza, serikali ya jiji la Buenos Aires imesema kuwa sanamu ya Lionel Messi itarekebishwa mara moja irudi katika muonekano wake wa awali.
Sanamu hiyo ni sehemu ya "the Paseo de la Gloria" kandokando ya fukwe za Rio de la Plata ambapo sanamu zingine za wanamichezo wa Argentina zipo kama vile mastaa Gabriela Sabatini, Manu Ginobili na Juan Manuel Fangio wanaenziwa pale

Sanamu la MESSI lavunjwa huko ARGENTINA Sanamu la MESSI lavunjwa huko ARGENTINA Reviewed by Unknown on Januari 10, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads