Header AD

Trump ayalaumu mashirika ya kijasusi ya nchi yake


Rais mteule wa Marekani Donald Trump ameshambulia mashirikia ya kijasusi nchini humo, huku akisema kwamba wangeweza kusababisha uvujaji wa tuhuma kwamba
Urusi imekusanya taarifa hatari kumhusu.
Trump ameyasema hayo katika mkutano wake wa kwanza na Waandishi wa habari.
Amevituhumu vile vile vyombo vya habari kwa kutoa taarifa alizoziita kuwa hazina ukweli ambazo amesema zimekusanywa na wagonjwa.
Mashirika hayo ya kijasusi yalimuarifu Trump na rais Obama kuhusu tuhuma hizo wiki iliyopita.
Trump ameendelea kusema kuwa, anatarajia kutakuwa na uhusiano mzuri kati yake na Vladimir Putin, lakini atahakikisha kwamba Marekani inaheshimika kimataifa kuliko ilivyo sasa.
Trump ayalaumu mashirika ya kijasusi ya nchi yake Trump ayalaumu mashirika ya kijasusi ya nchi yake Reviewed by Unknown on Januari 12, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads