Header AD

NIKOHURU BLOG# Kamanda Sirro :Tumemkuta Wema na Misokoto ya Bangi na Makaratasi Yake,Hivyo Naye Atapanda Mahakamani Tu ..!!






Sakata la wasanii 12 wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi limezidi
 kukua baada ya watu wengine 100 kukamatwa.
Kati ya watu 112 ambao wanashikiliwa na jeshi hilo 
kwa tuhuma za kujihusisha na utumiaji au biashara ya 
dawa hizo,
12 kati yao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo baada ya kazi hiyo kushindikana jana.

Miongoni mwa watuhumiwa wanaotarajiwa kupandishwa kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ni mwigizaji maarufu wa filamu Wema Sepetu na msanii mwenzake Omary Micheri ambao polisi wamedai walikutwa na vielelezo vya dawa za kulevya na bangi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
 Kamishna Simon Siro alisema watawafungulia watuhumiwa maombi ya kuwaweka chini ya uangalizi wa mahakama na polisi kwa muda 
wa miaka miwili na watakuwa wakiripoti kituo cha polisi mara 
mbili kwa mwezi.

Siro alisema kati ya watuhumiwa 12 waliokamatwa kwanza
, 10 walikiri kutumia dawa hizo na kuwataja wauzaji lakini wawili walikutwa na vielelezo nyumbani kwao.

Alisema Wema, ambaye aliwahi kushinda taji la mrembo wa
 Tanzania (Miss Tanzania), alipekuliwa nyumbani kwake
 na kukutwa na misokoto ya bangi na makaratasi yake, wakati
 Micheri alikutwa na kete tatu za dawa za kulevya ambazo 
hazijajulikana za aina gani hadi zitakapofanyiwa uchunguzi.

TIMU KAZI YA NIKOHURU BLOG ITAENDELEA KUKUPASHA HABARI KUNTU KATIKA NYANJA MBALIMBALI, HIVYO BASI NAWE MPENZI MSOMAJI WA BLOG YETU USISAHAU KUTU"FOLLOW INSTAGRAM , TWITTER na KU'LIKE PAGE YETU FACEBOOK
NIKOHURU BLOG# Kamanda Sirro :Tumemkuta Wema na Misokoto ya Bangi na Makaratasi Yake,Hivyo Naye Atapanda Mahakamani Tu ..!! NIKOHURU BLOG# Kamanda Sirro :Tumemkuta Wema na Misokoto ya Bangi na Makaratasi Yake,Hivyo Naye Atapanda Mahakamani Tu ..!! Reviewed by Unknown on Februari 07, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads