Header AD

Uingereza yakabiliwa na shinikizo la kufuta ziara ya Trump

media
Zaidi ya watu Milioni moja wametia saini waraka wa kuitaka Uingereza kusitisha ziara ya rais wa Marekani Donald Trump kuja nchini humo.
 wamesema kuwa, wamechukua hatua hii baada ya Trump kusitisha raia wanaotoka katika nchi za Kiislamu kuzuru Marekani.
Trump amealikwa Uingereza baadaye mwaka huu, kulihotubia bunge lakini pia kukutana na
 Malkia Elizabeth wa pili.
Juma lililopita Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May alikutana na rais wa Marekani Donald Trump, na walijadiliana kuhusu maswala mbalimbali yanayokumba nchi hizo mbili na dunia.
Kabla ya kukutana na rais Trump, Waziri Mkuu May alisema Uingereza itaendeleza urafiki wake wa karibu na Marekani, lakini alimuonya Trump kuwa karibu sana na Urusi, lakini pia kuendelea kusaidia katika 
vita dhidi ya ugaidi.
Theresa May ni kiongozi wa kwanza wa kigeni kukutana na rais Trump.
Akizungumza mjini Philadelphia, ikiwa ni mwanzo wa ziara yake nchini MarekaniBi May alisema kwa uhakika nchi yake ambayo ilimaliza uanachama wake kwenye Umoja wa Ulaya, iko tayari kujenga ushirikiano na marafiki zake wa zamani na wapya pia.
Uingereza yakabiliwa na shinikizo la kufuta ziara ya Trump Uingereza yakabiliwa na shinikizo la kufuta ziara ya Trump Reviewed by Unknown on Februari 08, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads