Header AD

NIKOHURU BLOG# PICHAZ: RAIS MPYA WA ZAMBIA AKIAPISHWA

Zaidi ya wananchi 60,000 wa Zambia hii leo wamefurika kwenye Uwanja wa National Heroes katika Mji Mkuu wa Zambia Lusaka kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Edga Lungu baada ya kuchaguliwa tena wakati wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika mapema Agosti mwaka huu.

Kuapishwa kwake kunafanyika baada ya upinzani kushindwa kwa kesi ya kutaka matokeo ya uchaguzi kubatilishwa, baada ya mahakama ya katiba kutupilia mbali kesi ikisema kuwa upinzani ulikuwa umeishiwa muda wa kupeleka suala hilo mahakamani.

Lungu alishinda uchaguzi wa Agosti 11 kwa asilimia 50.35 na kupita kiwango kilichowekwa ili kuepuka kurudiwa tena kwa uchaguzi.

Hakainde Hichilema ambaye alichukua nafasi ya pili kwa asilimia 47.63 anaendelea kupinga matokeo hayo akidai matokeo yalichakachuliwa.

NIKOHURU BLOG# PICHAZ: RAIS MPYA WA ZAMBIA AKIAPISHWA NIKOHURU BLOG# PICHAZ: RAIS MPYA WA ZAMBIA AKIAPISHWA Reviewed by Unknown on Septemba 14, 2016 Rating: 5

Post AD

Propellerads