Header AD

NIKOHURU BLOG#DIAMOND PLATNUMZ NA HARMONIZE NI BALAA…

Yawezekana umewahi kukutana na watu wa kukukatisha tamaa wakati wote, mara nyingi wamekwambia huwezi na kila ukijaribu unaishia kushindwa, sio mbaya kwani hakuna aliyezaliwa akiwa anajua ndio maana kwenye maisha kuna nafasi ya pili ya kujaribu tena na tena ili ufanikishe kile unachokitaka.diamond

Reshma Qureshi ni mwanadada mwenye ulemavu asiye na jicho moja ambaye ameshiriki katika mashindano ya urembo jijini New York licha ya ulemavu alionao; unaweza kujiuliza inawezekana vipi dada kama huyu na mapungufu aliyonayo akaamua kushiriki shindano kubwa la urembo kama hilo? Jibu ni kwamba amejikubali kisha akajiamini kwamba anaweza.reshma-qureshi

Wapo watu wengi mashuhuri ambao kwa sasa wanafanya vizuri licha ya kukatishwa tamaa katika mwanzo wa safari yao; Diamond Platnumz na Harmonise ni mmoja wa waliokatishwa tamaa lakini kwa kuwa walikuwa ving’ang’anizi na wabishi ili wafanikiwe waliendelea kukaza hadi wakafanikiwa na kutusua kimuziki.

Wakati Diamond anapambana kutoka kimuziki alipokutana kwa mara ya kwanza na Papaa Misifa wapo baadhi ya watu waliotilia shaka uwezo wake kiuimbaji na kumtaka akomae, halikadhalika kwa Harmonise aliposhiriki katika Shindano la BSS 2012 mmoja wa majaji wa shindano hilo ambaye pia ni Producer mkubwa hapa Bongo maarufu kama Master J alimchana Harmonise kwamba hajui kuimba.harmonize and diamond

Kitendo cha msanii huyo kuambiwa hivyo hakikumkatisha tamaa bali kilimuongezea hasira za kupambana zaidi na zaidi. Hili ni darasa tosha kwa yeyote ambaye anakatishwa tamaa, unakila sababu ya kupigana ili kuyafikia mafanikio yako kwani waliokatishwa tamaa hii leo wamefanikiwa, hupaswi kukata tamaa unachopaswa ni kukubaliana na hali iliyopo huku ukibuni mbinu mpya za kupambana kila uchwao ili utoboe.(mtembezi.com)


Usisahau ku"share" habari hii kwa rafiki zako

NIKOHURU BLOG#DIAMOND PLATNUMZ NA HARMONIZE NI BALAA… NIKOHURU BLOG#DIAMOND PLATNUMZ NA HARMONIZE NI BALAA… Reviewed by Unknown on Septemba 14, 2016 Rating: 5

Post AD

Propellerads