Header AD

NIKOHURU BLOG#WCB Waonyesha Jinsi Walivyomalizana na Uongozi wa Saida Karoli ili Kurudia Wimbo wa Salome

Sallam kutoka WCB ameonyesha baadhi ya nyaraka ambazo zimewapitia kibali cha kutumia sehumu za wimbo ‘Maria Salome’ wa Saida Karoli katika wimbo mpya wa Diamond, ‘Salome’. 
Wimbo ‘Maria Salole’ wa Saidi Karoli ni miongoni mwa nyimbo za asili zilizofanya vizuri miaka ya 2000.
 
Hali hiyo iliufanya uongozi wa Diamond kuzungumza na uongozi wa Saida Karoli ili upate kibali cha kutumia sehemu za nyimbo hiyo.
 
“Tunakushukuru sana uongozi wa Saida Karoli na mzee Felician Mutakyawa kutupa haki na baraka zote kutumia wimbo wa Maria Salome,” aliandika Sallam instagram. “Tunatambua kwamba nyimbo hii itaendelea kuwa moja ya nyimbo bora kuwahi kutoka katika nchi ya Tanzania,”
 
Diamond kupitia wimbo huu amerudi tena katika nyimbo za asili baada ya kufanya vizuri na wimbo ‘Mdogo Mdogo’ miaka miwili iliyopita.

NIKOHURU BLOG#WCB Waonyesha Jinsi Walivyomalizana na Uongozi wa Saida Karoli ili Kurudia Wimbo wa Salome NIKOHURU BLOG#WCB Waonyesha Jinsi Walivyomalizana na Uongozi wa Saida Karoli ili Kurudia Wimbo wa Salome Reviewed by Unknown on Septemba 20, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads