Header AD

Kamanda Sirro: Wema Sepetu, Nyandu Tozzy na TID bado wanashikiliwa na jeshi la polisi

Wakati macho na masikio ya Watanzania wakisubiri kusikia hatma ya wasanii wanaodaiwa kujihusisha na dawa za kulevya, wasanii wanne waliofika Kituo Kikuu cha Polisi bado wanashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano zaidi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa bado wasanii hao Wema Sepetu, Dogo Hamidu, Khalid Mohamed (TID), na mtangazaji maarufu wa Clouds TV Babuu wa Kitaa bado wanashikiliwa na jeshi hilo.

“Bado tunawashikilia kwa mahojiano zaidi,” amesema Sirro kwa kifupi.

Wasanii wengine waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambao wanatakiwa kufika kituoni Jumatatu ni Vanessa Mdee, Tunda na watu wengine Halidali Kavila, Amani, Kashozi na Omry Sanga.

Kamanda Sirro: Wema Sepetu, Nyandu Tozzy na TID bado wanashikiliwa na jeshi la polisi Kamanda Sirro: Wema Sepetu, Nyandu Tozzy na TID bado wanashikiliwa na jeshi la polisi Reviewed by Unknown on Februari 05, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads