Header AD

Kampuni ya Mo Dewji, Lamada Hotel ni mdaiwa sugu wa kodi.....maofisa Ardhi wavamia ofisi, Watoa Notisi ya Siku 14

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza oparesheni maalumu ya kukusanya Kodi ya Pango la Ardhi kutoka kwa wadaiwa sugu wa Makampuni, mashirika ya kiserikali na watu binafsi kwa kuwafuata katika maeneo yao.

Katika hatua ya kwanza Wizara kwa kushirikiana na Manispaa za  mkoa wa Dar es salaam imetoa notisi kwa wadaiwa sugu wa kodi ya pango la Ardhi wakiwemo Mohammed Enterprises anaedaiwa Shilingi milioni 73, Lamada  Hotel anaedaiwa Shilingi milioni 54, Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) anaedaiwa Shilingi milioni 144 na Tanganyika Motors anaedaiwa Shilingi milioni 22.

Makampuni hayo yamepewa notisi ya siku 14 ili kulipa kodi hizo wanazodaiwa na endapo hawatalipa watafutiwa umiliki au mali zao kwa kupigwa mnada ili kufidia gharama wanazo daiwa.

Serikali kwa kutumia kampuni ya Udalali ya Msolopa Investment imeendesha oparesheni hiyo kwa kufika katika ofisi za wamiliki wa viwanja na mashamba makubwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Akiongea kwa kusisitiza, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila amesema katika mwaka wa fedha 2016/17 Wizara imepanga kukusanya Sh. bilioni 111.77 kutokana na Kodi ya Pango la Ardhi.

Wizara haitaweza kufanikisha malengo hayo endapo itaendelea kuwaachia wadaiwa sugu ambao hawataki kulipa kodi. Kwani kwa miaka mingi sasa mapato mengi ya serikali yamekuwa yakiachwa kutokana na kushindwa kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi Kayandabila alisisitiza.

Baadhi ya watumishi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kampuni ya Udalali ya Msolopa Investment na baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa nje ya Ofisi ya Mohammed Enterprises iliyopo jingo la Golden Jubilee mara baada ya wafanyakazi wa Mohammed Enterprises kukimbia.

Wafanyakazi wa Lamada Hotel (kushoto) wakiangalia kwa makini Notisi ya madai ya kodi ya Ardhi wakati ikiwasilishwa na watumishi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na kampuni ya Udalali ya Msolopa Investment.

Watumishi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na kampuni ya Udalali ya Msolopa Investment wakiwa nje ya ofisi Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) ili kuwasilisha notisi ya madai ya kodi ya ardhi. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila akiongea na waandishi wa habari kwamba Serikali kupitia Wizara yake haitamuacha mtu au kampuni yoyote inayodaiwa kodi ya Ardhi hata kama ni Taasisi ya serikali.

Hassan I. Mabuye
Information Officer
The Ministry of Lands, Housing
and Human Settlements Development

Dar es salaam, Tanzania

Kampuni ya Mo Dewji, Lamada Hotel ni mdaiwa sugu wa kodi.....maofisa Ardhi wavamia ofisi, Watoa Notisi ya Siku 14 Kampuni ya Mo Dewji, Lamada Hotel ni mdaiwa sugu wa kodi.....maofisa Ardhi wavamia ofisi, Watoa Notisi ya Siku 14 Reviewed by Unknown on Februari 05, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads