Header AD

NIKOHURU BLOG# Mahakama Zambia kuamua iwapo Rais Lungu atagombea tena urais au la!

Mahakama ya Katiba ya Zambia imetangaza tarehe 21 mwezi huu wa Februari kuwa siku ya kusikiliza kesi ya wapinzani nchini humo wanaotaka ufafanuzi wa kikatiba kuhusu iwapo
Rais Edgar Lungu wa nchi hiyo anafaa kuwania urais kwa muhula wa tatu au la mwaka 2021.
Hakimu Margaret Munalula wa Mahakama ya Katiba Zambia anatazamiwa kutoa uamuzi huo nyeti Februari 21, uamuzi ambao utatoa mwangaza kuhusu mustakabali wa siasa za nchi hiyo ya Afrika.
Kesi ya kutaka ufafanuzi wa kikatiba kuhusu suala hilo iliwasilishwa mahakamani na wanasiasa wakuu wa vyama vya upinzani, wakiwemo Daniel Pule wa Christian Democratic Party, Wright Musoma wa Zambian Republican Party, Rais wa New Congress Party Peter Chanda, na Robert Mwanza wa Citizens Democratic Party. 
Mapema mwezi uliopita wa Januari, kauli ya Rais Lungu kwamba atagombea tena urais kwa muhula wa tatu katika uchaguzi ujao nchini humo, iliibua mjadala mkubwa miongoni mwa kambi ya wapinzani na hata ndani ya chama tawala anachokiongoza.


Rais Edgar Lungu wa Zambia

Rais Lungu aliyeshinda uchaguzi wa rais wa mwezi Agosti mwaka jana ikiwa ni muhula wa pili na wa mwisho wa uongozi wake kwa mujibu wa tafsiri ya wapinzani ya katiba, hivi karibuni alitangaza kwamba atagombea tena uchaguzi wa mwaka 2021 na kwamba mahakama ya katiba ya nchi hiyo pia inafahamu vyema kuwa hiyo ni haki yake.
Rais Edgar Lungu aliingia madarakani kwa muhula wa kwanza ikiwa ni kukamilisha muhula wa uongozi wa Rais aliyemtangulia, Michael Sata ambaye alifariki dunia kabla ya muhula wa miaka miwili ya uongozi wake kumalizika.
Baadaye Lungu alimshinda Hakainde Hichilema, mgombea wa upinzani wa chama cha UPND, uchaguzi ambao hata hivyo uliibua sutafahumu kubwa kufuatia kambi ya upinzani kupinga matokeo kwa kile ilichokisema kuwa ni uchakachuaji uliofanywa kwenye uhaguzi huo.  
NIKOHURU BLOG# Mahakama Zambia kuamua iwapo Rais Lungu atagombea tena urais au la! NIKOHURU BLOG# Mahakama Zambia kuamua iwapo Rais Lungu atagombea tena urais au la! Reviewed by Unknown on Februari 06, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads