Header AD

Cameroon Bingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2017

Timu ya Taifa ya Soka ya Cameroon imetawazwa kuwa mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka 2017 baada ya kuilaza timu ya Taifa ya Misri kwa mabao 2-1.

Ushindi wa timu ya taifa ya Soka ya Cameroon umepatikana katika fainali za mashindano hayo yaliyofanyika nchini Gabon na ni ubingwa wa mara ya tano kwa ujumla kwa Cameroon na wa kwanza wa timu hiyo tangu mwaka 2002.
Katika mechi hiyo iliyofuatiliwa na mashabiki wengi wa soka barani Afrika na maeneo mengine ya dunia, Misri ndiyo iliyokuwa ya kwanza kutikisa nyavu za Cameroon baada ya kiungo wa timu ya Arsenal ya Uingereza, Mohamed Elneny kufunga goli kwa shuti kali katika dakika ya 21. 


Timu ya taifa ya Cameroon

Dakika ya 58, Nicolas N'Koulou alijibu mapigo kwa kufunga bao la kusawazisha la Cameroon kwa kichwa, kabla ya Vincent Aboubakar kuwahakikishia ubingwa Simba wa Cameroon, The Indomitable Lions, kwa kupachika wavuni bao la pili katika dakika ya 88 na hivyo kuzamisha kabisa jahazi la Mafarao.


Mashabiki wa timu ya soka ya Cameroon

Ubingwa wa mwaka huu wa Cameroon unaandika rekodi mpya na ya kwanza baada ya timu hizo kukutana katika hatua ya fainali mwaka 1986 na 2008, ambazo zote Misri iliibuka mbabe.
Cameroon Bingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2017 Cameroon Bingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2017 Reviewed by Unknown on Februari 06, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads