Trump : 'Namheshimu Rais wa Russia Vladimir Putin, lakini…'
Rais Donald Trump amesema ijapokuwa “anamheshimu”
Rais wa Russia Vladimir Putin sio lazima kuwa
mtangamano wao utadumu.
“Lakini nasema ni bora kushirikiana na Russia kuliko vinginevyo
. Na kama Russia itatusaidia katika kupambana na kundi la
Islamic State, ambayo ni vita kubwa, na ugaidi wa kiislamu dunia
nzima—
hilo ni jambo zuri,” Trump ameliambia shirika la Televisheni
la Fox News katika mahojiano yake ambayo yatatangazwa Jumapili.
“Je nitaweza kushirikiana naye? Sina wazo lolote kuhusu hilo.”
Udhalimu wa Putin
Alipoulizwa kuhusu mauaji alioyafanya Putin siku za nyuma, na jinsi gani Trump angeweza kumheshimu
hata baada ya kujua historia yake, Trump ameifananisha Russia na Marekani.
“Kuna wauaji wengi. Sisi pia tunao wauaji wengi. Unafikiria nini? Nchi yetu haina makossa? amesema
hayo, kwa mujibu wa sehemu ya maelezo hayo yaliyo patikana kutoka katika mahojiano yake na
Fox News siku ya
Jumapili.
Kiongozi wa Baraza la Seneti
Akijibu juu ya maoni haya ya Trump kwenye televisheni ya CNN, kiongozi wa wengi katika Baraza la
Seneti Mitch McConnell amesema yeye hafikirii “tunaweza kuilinganisha” Marekani na Putin.
Mashirika ya kipelelezi Marekani yameishutumu Russia kwa udukuzi wa kompyuta zilizokuwa zikitumiwa na
Chama cha Demokratik kama njama ya kampeni pana za Russia kuvuruga uchaguzi wa urais wa Marekani.
Kabla ya kuchukuwa madaraka, Trump alirejea mara nyingi kudadisi taarifa za jumuiya ya kipelelezi. Lakini
ukosoaji wake umesita kwa muda sasa. Bado, rais ameendelea kusema hadharani kwamba yuko
tayari kwa mahusiano bora na Moscow.
Mazungumzo ya Trump na Putin
Trump na Rais wa Russia walikuwa katika mazungumzo ya simu siku ya Jumamosi katika kile
White House ilichokiita kama “ ni mwanzo muhimu katika kuboresha mahusiano kati ya Marekani na
Russia jambo ambalo lilikuwa linahitaji hatua hiyo.”
Vipande ya mahojiano hayo vina swali linalo ongelea agizo la Trump kuhusu uchunguzi wa wizi wa
kura katika uchaguzi wa urais Novemba.
Madai dhidi ya Hillary
Trump amedai mara nyingi kuwa wahamiaji haramu walopiga kura wamemzuilia kupata kura ya
umaarufu. Trump alishinda kura za wajumbe “Electoral College” lakini alipoteza kura za umaarufu kwa
idadi ya kura
milioni 2.9 ambazo zilichukuliwa na mgombea wa Demokratik Hillary Clinton katika uchaguzi mkuu mwaka
jana.
“Nataka niwaambie unapoona wahamiaji haramu – watu ambao sio raia na wapo katika usajili wa
kupiga kura,” Trump amesema. “Utawaona wahamiaji haramu, wako watu waliokwisha kufa, una haya
yote, ni hali mbaya sana, kwa kweli ni mbaya.”
Hata hivyo maafisa wa uchaguzi ambao walizichambua kura za Novemba 8 wanasema hakukuwa na dalili
yeyote ya wizi wa kura, kwa kweli sio katika kiwango kinachoelezewa na Trump.
Trump : 'Namheshimu Rais wa Russia Vladimir Putin, lakini…'
Reviewed by Unknown
on
Februari 06, 2017
Rating:
Post a Comment