Header AD

NIKOHURU BLOG# Serikali kujenga vituo vya polisi wilaya 65


NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI, HAMAD YUSUPH MASAUNI.
SERIKALI imekusudia kujenga vituo vya polisi katika wilaya 65 ambazo hazina vituo hivyo, lakini pale itakapopata fedha kupitia njia zake za mapato.



Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuph Masauni, alisema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Esther Midimu, kuwa kwa sasa serikali ya Muungano yenye wilaya 162, ina vituo vya polisi katika wilaya zake 97.

Masauni alisema kwa sasa serikali imefanikiwa kupata jengo wilayani Maswa ambalo litatumika kama kituo cha polisi cha wilaya huku wakisubiri utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa vituo vya polisi nchi nzima.

Hata hivyo, Masauni alimwomba mbunge huyo kuwa na subira, wakati serikali ikitafuta fedha za kukamilishia vituo vya polisi katika wilaya zote zilizosalia ikiwamo ya Maswa.

Awali, Mbunge Midimu, alitaka kujua pamoja na ukongwe wa wilaya ya Maswa iliyoko mkoani Simiyu, kwa nini serikali haina mpango wa ujenzi wa kituo cha polisi cha wilaya.


NIKOHURU BLOG# Serikali kujenga vituo vya polisi wilaya 65 NIKOHURU BLOG# Serikali kujenga vituo vya polisi wilaya 65 Reviewed by Unknown on Februari 04, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads