Header AD

Serengeti Boys Yafuzu Kucheza Fainali za U -17 baada ya kushinda rufaa yao dhidi ya "kijeba" wa Congo

Tanzania imefuzu kwa mara ya kwanza kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana U-17 zitakazofanyika Gabon mwaka huu.

Serengeti Boys ilifuzu baada ya kushinda rufaa yake dhidi ya Congo iliyomchezesha mchezaji aliyezidi umri.

Tanzania itaingia Kundi B ikichukua nafasi ya Congo kundi hilo lina timu za Niger, mabingwa watetezi Mali na Angola.

Timu nne zinazofanikiwa kuingia katika nusu fainali zitafuzu moja kwa moja  Kombe la Dunia la Fifa U17 litalofanyika India baadaye mwaka huu.

Waziri wa Michezo, Nape Nnauye aliandika kwenye akaunti yake ya twiter kuipongeza Serengeti Boys kwa kufikia hatua hiyo.

“Mungu Mkubwa! Tumefuzu kwenye fainali za Afrika chini ya umri wa miaka 17. Nia, uwezo na sababu za kuchukua kombe hili tunazo. Hongera TZ” aliandika Nape.
Serengeti Boys Yafuzu Kucheza Fainali za U -17 baada ya kushinda rufaa yao dhidi ya "kijeba" wa Congo Serengeti Boys Yafuzu Kucheza Fainali za U -17 baada ya kushinda rufaa yao dhidi ya "kijeba" wa Congo Reviewed by Unknown on Februari 04, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Post AD

Propellerads